Lello Mmassy
Ni Mchumi Kitaaluma, akiwa na Shahada katika Maendeleo ya Uchumi aliyohitimu kutoka Chuo Kikuu Cha Mwalimu Nyerere kinachopatikana Dar es Salaam, Tanzania. Kikazi, Lello ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Wateja katika kampuni ya Utengenezaji wa Vinywaji ya Tanzania Breweries Limited (TBL). Lello ameandika vitabu kadhaa mashuhuri ambavyo baadhi vimeshinda tuzo ya ubora wa Fasihi ya Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African Literature kwa kitabu chake cha Mimi na Rais. Vilevile, Lello Mmassy ni Mwanzilishi wa Programu tumishi iitwayo Simulizi Africa inayopatikana katika duka la programu la Google, ‘Playstore’ na pia ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Serengeti Bytes inayojishughulisha na Mahusiano kwa Umma, Masoko, Uchapishaji, na Vyombo vya Habari.
Lello ni mpenzi na mfuatiliaji mkubwa wa masuala ya Fasihi ya ndani na nje ya Afrika.